Saturday 23 April 2016

Mtoto wa Miaka 16 Kutoka Tanzania amehutubia Mbele ya Marais 60 Duniani

Binti wa Miaka 16 Kutoka Mwanza Ahutubia Umoja wa Mataifa


Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza Amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo Anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.

Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana‘

Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza kuwawakilisha vijana na watoto ambapo Alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko ha

No comments:

Post a Comment