Friday 29 April 2016

Rufaa ya Michael Platini Kuamuliwa Wiki Ijayo

 

 

Rais wa Uefa aliyesimamishwa Michel Platini alionekana mbele ya Mahakama ya Juu Zaidi ya Michezo CAS Siku ya Ijumaa kwa ajili ya kukata Rufaa Dhidi ya kupigwa Marufuku ya Miaka Sita kutojihusisha na Soka huku akisema anamatumaini atashinda kesi yake.

Platini, ambaye aliwasili kwa Teksi kwa ajili ya kusikilizwa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS), anatarajia kuwa Hatua hiyo itapindua Maamuzi hayo na kumwezesha kuhudhuria Mashindano ya Euro 2016 Yatakayofanyika Ufaransa ambayo ni nchi yake ya Nyumbani.

CAS imesema Uamuzi wa Rufaa hiyo Unaweza kutolewa Mapema Wiki ijayo kutokana na kutengewa Muda Mrefu wa kusikilizwa.

Platini alipigwa marufuku kwa miaka nane mwezi Desemba pamoja na Blatter kutokana na Tuhuma ya Matumizi Mabaya ya Pesa na Madaraka.

No comments:

Post a Comment