Thursday 28 April 2016

Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Wamempongeza Rais Dkt John Magufuli Ujenzi wa Bomba la Mafuta

 

Na Mwamvita Mtanda

Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) pia kimeipongeza timu ya mazungumzo iliyoongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, huku kikiwataka Wanachama wake na wadau wote kwa ujumla kuchangamkia fursa nyingi na kubwa za Kibiashara zitakazotokana na Ujenzi wa Bomba hilo.

“Tunatoa shukrani zetu za Dhati kwa rais wetu na timu iliyoshiriki kwenye Mazungumzo, Wametufanyia Jambo kubwa katika Ujenzi wa uchumi wa nchi…imebaki Juu yetu kupanga Mikakati ya namna ya kutumia fursa za kibiashara zitakazoletwa na Mradi huu,” alisema Mwenyekiti wa Tatoa, Angelina Ngalula jijini Dar es Salaam

Ngalula alisema kutokana na fursa hii kubwa iliyopatikana, Wadau wote wa Bandari wana Wajibu wa kuitumia katika kutangaza Bandari Zilizopo nchini ili kuvutia wawekezaji na Wateja katika kukuza Uchumi wa nchi.

“Fursa hii kubwa itaifanya Bandari ya Tanga kuingia katika Ramani ya Dunia hivyo basi ni Vyema Wadau wote wa Bandari na Wapenda maendeleo kuitumia Vizuri Nafasi hii,” alisema Mwenyekiti na kuongeza kuwa Utekelezaji wa Mradi huo wa Bomba lenye urefu wa kilometa 1,403 kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga Utatengeneza fursa nyingi za Usafirishaji Mizigo kwa njia ya Reli na Barabara.


No comments:

Post a Comment