Friday 29 April 2016

Jaji Mkuu Othumani Chande Mgeni Rasmi Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mei 3


 

 Na Tabu Mullah

Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho Ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yatakayofanyika Mei 3, Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari  Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania, Simon Berege, alisema Maadhimisho hayo Yatafanyika kitaifa Mkoani Mwanza yakiwa na kaulimbiu isemayo ‘Kupata Taarifa ni haki Yako ya msingi,

Alisema, Maadhimisho ya Mwaka huu Yatawashirikisha Watu 250 kutoka ndani na nje ya Nchi, Watakaojadili Mambo Mbalimbali Yanayohusu Haki ya kupata habari na Uhuru wa Vyombo Vya habari Tanzania.

Alisema, Maadhimisho hayo yatatumika kutafakari namna gani Tanzania imetoa Uhuru kwa Vyombo vya habari, kupitia sheria mbalimbali Juu ya Vyombo vya Habari pamoja na kuwakumbuka wanahabari wote Waliopoteza Maisha wakiwa kazini.

Berege alisema Maadhimisho ya Mwaka huu ni muhimu kwani yameendana na maadhimisho Ya karne Mbili na Nusu za kupata Habari Duniani. Pia, alisema katika Maadhimisho hayo, 

MISA Tanzania itazindua chapisho lake kwanza litakalojulikana kama ‘So this is democracy?’
Kwa Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alisema, kutatolewa Misimamo Mbalimbali Juu ya hali ya uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini

No comments:

Post a Comment