Sunday 24 April 2016

Ijue Timu ambayo itavaana na Yanga fc Katika Klabu Bingwa Afrika



 Na Mwamvita Mtanda

Grupo Desportivo Sagrada Esperança, kwa ufupi inajulikana kama Sagrada Esperança au GD Esperança. Inatoka katika mji wa Dundo, ulioko jimbo la Lunda Norte, Kaskazini ambako imeanzishwa Desemba 22, mwaka 1976.

Inaaminika kuwa asili ya jina hilo imetokana na shairi la la Rais wa kwanza wan nchi hiyo Agostinho Neto lililojulikana kama Sagrada Esperança Ikimaanisha (Sacred Hope) au tumaini lenye utakaso.

Timu hii ilianzishwa na kampuni ya madini ya Almas ambayo kwa sasa inafahamika kwa jina la Endiama ambayo kwa sasa ndiyo mdhamini mkuu wa klabu hiyo Kama ilivyo ilivyo Mwadui FC kwa hapa Tanzania.

Kombe lake la kwanza tangu kuanzishwa ililipata mwaka 1988, ikiwa ni Angolan Cup ambalo ni kama ilivyo kombe la FA nchini England au Kombe la Shirikisho kwa Tanzania.

Mwaka 2005 iliweza kubeba ndoo ya ligi kuu nchini humo kwa mara ya kwanza nay a mwisho na katika mwaka huo iklishiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kutolewa na Asec Abidjan ya Ivory Coast katika hatua ya 16 bora.

Ina uwanja wake ambao ulizinduliwa mwaka 2008, unaitwa Estádio Sagrada Esperança katika mji wa Dundo una uwezo wa kubeba watu 8000.

Timu hii inashiriki ligi kuu ya Angola inayofahamika kwa jina la Girabola na mwaka 2008 ilishuka daraja ilishiriki ligi daraja la kwanza nchini humo na baadaye kurejea tena ligi kuu.

HISTORIA YAKE KATIKA MICHUANO YA AFRIKA
Michuano wa Klabu Bingwa Afrika imeshiriki mara 2 pekee, ambapo mwaka 2005 iliishia Raundi ya kwanza na mwaka 2006 ilitolewa mapema kabisa katika hatua ya awali.

Katika michuano ya Shirikisho, mbali na mwaka huu, mwaka 1992 iliishia raundi ya 2 na Mwaka 1998 iliishia raundi ya kwanza, ambapo katika mwaka huu, Yanga ilifika hatua ya Makundi.

Wakati ule bado kulikuwa na kombe la washindi ambako pia ilishiriki mara 2, mwaka 1989 na mwaka 2000 na mara zote iliishia raundi ya 2.

KOCHA
Ina historia ya kukaa na kocha kwa mwezi mmoja pekee, ambapo mwaka jana, ilimuajiri Kochas Frank Moniz mwezi machi na kumtimua mwezi April mwaka huohuo, na baadaye ikamchukua Zoran Mackic ambaye alimaliza nayo msimu ikiwa katika nafasi ya 10 ya Msimamo wa ligi.

MAFANIKIO YAKE NDANI YA ANGOLA
Imefanikiwa kutwaa taji la Girabola mara moja (2005) pamoja na Kombe la Angola (FA ya Angola) mara mbili mwaka 1988 na 1999.

No comments:

Post a Comment