Thursday 28 April 2016

Yanga Yaota Ubingwa Tanzania Bara ligi Kuu ya Vodacom


 

 Na Mwamvita Mtanda

Miaka 81 Tangu Dar es Salaam Young Africa izaliwe imefanya Mengi mno katika soka la Ndani, Yanga ama Simba Zinapokaribia kumaliza ligi kila Mmoja ana Namna yake ya kumaliza ligi Wengi huwaacha hoi. Mfano wake kama Umewahi kuwaona Wachimbaji Madini Pindi Wanapohisi Dhahabu iko karibu anafanya Haraka na anatumia Nguvu nyingi huku Akijua kuwa akipata Dhahabu Utajiri uko mbele yake.

Yanga imetoka katika Sintofahamu ya Mchezo wake Dhidi ya Coastal Union Baada ya Mwamuzi Wa Pambano hilo kugushi Maamuzi yake na kupewa lawama kuchezesha chini ya kiwango Ambapo kamati ya Maadili imetoa maamuzi kuwa Yanga imeingia hatua ya Fainali na itacheza Na Azam FC.

Yanga kama kauli ya Jeri Muro anavyoita klabu hiyo kuwa Wakimataifa Jana imeichapa Mgambo JKT 2-1 na kuzidi kuwaacha mbali Simba na Azam kama Walivyo Wakenya katika Riadha Yanga Sasa Wamefikisha alama 62 huku Azam alama 58 na Simba alama 57 Michezo 25 Huku Yanga akiwa na Magoli 45 Azam 27 na Simba 29. Michezo mengine ulikuwa wa Azam Na Majimaji ambapo Azam imeshinda 2-0.

No comments:

Post a Comment