Monday, 18 April 2016

Simon Siro:Kuwaondoa Ombaomba Dar Tutafuata Haki Zote za Binadamu Zinazostahili Kuzipata

 

Imepita wiki moja tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alipotangaza kuwa Ombaomba wote inabidi waondolewe maeneo ya mjini, macho na masikio ya watanzania yalikuwa yanasubiri kitakacho fanyika leo Jumatatu ya Aprili 18, katika zoezi la kuwaondoa ombaomba Jijini hapa.

Wakati Watanzania wakisubiri hatua zitakazo chukuliwa na Jeshi la Polisi katika kuwaondoa Ombaomba, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es Salaam Simon Sirro amesema hawatalianza zoezi hilo mpaka watakapo fanya taratibu stahiki kwa kuzingatia haki za binadamu.

 

Kamanda Sirro amesema zoezi la kuwaondoa Ombaomba litahusisha kamata kamata, hivyo kuna utaratibu wa kuwakamata tofauti na unavyo wakamata watu wengine mfano Majambazi, Wafanyabiashara ya ngono (Dada poa, Kaka poa) na wahalifu wengine.

 

 

Vilevile Kamanda Sirro ameeleza kuwa zoezi la kuwaondoa ombaomba ni suala Mtambuka Hivyo litahusisha Idara na Wizara mbalimbali kwa pamoja kwa kuwa Ombaomba hawa Watahitaji Chakula na Usafiri, katika hatua nyingine Kamanda Sirro amesisitiza kuwa zoezi la kuwaondoa ombaomba siyo nguvu ya soda, hivyo ni bora waondoke bila nguvu ya Jeshi la Polisi kwani siyo vizuri.

No comments:

Post a Comment