Friday 22 April 2016

Malaika:Kuandika Nyimbo ni Kipaji Sio Kila mtu anaweza Kuandika

malaika_rarua_rarua
MaMlaiAmesema anaamini kuwa uandishi wa nyimbo ni kipaji Ambacho si kila mtu anacho na kwamba ukiwa nacho ni mali.


“Unajua uandishi wa nyimbo ni kipaji na si kila mtu anacho. Kwa msanii ukiwa nacho ni raha maana itakurahisishia kazi yako na siyo Hadi usubiri kupata mtu akuandikie, inachukua muda sana,” amesema.
“Unaweza kukuta huyo mtu naye yupo busye na mambo yake, unakuta Msanii unakuwa sometimes huwezi kutoa kazi zako kwa muda ambao umepanga,” ameongeza.
Amesema wimbo wake mpya Raruararua ameuandika mwenyewe lakini verse ya mwisho imeandikwa na Rich Mavoko. Kwa upande Mwingine amesema video ya wimbo huo imeshakamilika.
“Nadhani kuanzia wiki ijayo itatoka na kubadilika kwa tokea nilivyoanza kwa kazi zangu kama, Nenda, Mwantumu, Zogo Sare Sare.”
“Unajua msanii lazima uwape ladha tofauti mashabiki wako maana kila mtu na anachopenda. Kama huwa nikipata muda wa kuongea na Mashabiki wangu, unakuta kila mtu anakwambia ‘mimi napenda sana wimbo wako fulani’ kwahiyo nadhani ni vizuri kwa msanii kwani unakuwa na mashabiki tofauti tofauti.”

No comments:

Post a Comment