Friday 29 April 2016

TCRA: Baadhi ya Wauzaji wa Simu Wanatoa Punguzo Kwa Wananchi ili kuwashawishi Kununua Simu Bandia kwa Bei Nafuu

 

  Na Kalonga Kasati

Tarehe  April 23 Mwaka huu China ilizifungia Huduma za kampuni ya Apple katika mtandao Pamoja na zile za filamu katika Harakati ya kuweka Sheria kali Zitakazosimamia kile kitakachochapishwa Mtandaoni.

Nchi nyingi Duniani zimeridhia kupitisha Sheria ya Makosa ya Mtandao, lengo kuu likiwa ni Udhibiti wa Uhalifu Mitandaoni na kuendelea kuboresha Teknolojia kadri inavyoendelea kukua, Desemba 17 Mwaka Jana Ulizinduliwa Mfumo wa Uhifadhi namba Tambulishi za vifaa Vya Mawasiliano kwa Simu za Mkononi (IMEI) kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi kwa Vifaa Vinavyoibiwa na vile Visivyokidhi Viwango.

Akibainisha kazi zilizofanyika tangu kuzinduliwa kwa mfumo huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema  Mamlaka hiyo imeendelea kufanya Uchambuzi wa kina ilikupata mwelekeo halisi kabla ya kipindi kilichowekwa kuisha na Hatimaye simu ambazo hazikukidhi vigezo kuzimwa rasmi Juni 17 Mwaka huu.

“Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendelea kusimamia kwa karibu makampuni ya simu Hapa nchini katika uendeshwaji wa kila siku wa mfumo wa rahisi za namba za utambulisho wa Vifaa vya mawasiliano vya mkononi, ili kupata mwelekeo halisi kabla ya kipindi cha mpito kuisha  Juni 17, mwaka huu”. Alisema Kilaba

Pamoja na hayo changamoto inayokabili mfumo huo ni pamoja na uaminifu mdogo kwa Baadhi ya wauzaji wa simu kwa kutoa punguzo kwa wananchi ili kushawishi kununua simu Bandia kwa bei nafuu.

No comments:

Post a Comment