Saturday 30 April 2016

Simon Group Inamiliki UDA Asilimia 51 na Serikali 49



 Na Mwamvita Mtanda

Umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa Jiji la Dar es Salaam, umekoma Rasmi Baada ya Kampuni ya Simon Group kukamilisha Malipo ya Ununuzi wa Hisa za jiji hilo katika Shirika hilo ambazo ni asilimia 51.

Kutokana na kukamilika kwa Malipo hayo, sasa Uda inamilikiwa Kampuni ya Simon Group Yenye asilimia 51 ya hisa ambazo ndizo Zilizokuwa Hisa za Jiji na Serikali yenye asilimia 49.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru alisema Mpaka katikati ya Aprili, mwaka huu, Kampuni ya Simon Group ilikuwa imemaliza kulipia Malipo ya Hisa zote Zilizokuwa Zikimilikiwa na Jiji.

Kwa Mujibu wa Mafuru, sasa Serikali inapaswa kuitambua Kampuni ya Simon Group kuwa Mwenye hisa katika Shirika hilo, kwa kuwa kampuni hiyo imewasilisha Nyaraka za Ununuzi wa Hisa hizo na Jiji limethibitisha kupokea fedha zao na kukubali kwamba Muamala huo wa Malipo ni halali.

Akifafanua namna ununuzi huo ulivyo halali, Mafuru alisema Jiji walifungua kesi kuomba Mahakama iagize Kampuni ya Simon Group ilipe fedha za hisa za Jiji kufikia Aprili 30 Mwaka Huu, kinyume cha hapo Hisa hizo Zirudishwe kwa Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment