Sunday, 7 February 2016

PPF Wakabidhiwa Rasmi JengoJipya La Kisasa Walilojenga Jijini Arusha Lenye Thamani Ya Bilioni 32.5

Kiongozi Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo,  Arch. Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya   MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.

 Na Tabu Mullah
DG William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha kukamilika kwa Mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika Bajeti iliyopangwa Mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha miradi ya PPF Makao makuu, wabunifu na Wasimamizi, Mamlaka za Jiji, idara nyingine za Serikali na Wakandarasi Wenyewe. 

Jengo hilo Maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye Ghorofa 10 sambamba na Eneo la Basmenet yenye Uwezo wa kupaki Magari 168, lina thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina Huduma zote Muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo ‘lifti’ za kutosha, Majenereta makubwa, Mataki ya Maji na mafuta ya Jenerata, mfumo wa kukabiliana na Moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha Magari ndani ya Jengo.
Kwa mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018 ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo imewachukua miaka Miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika ubora wa kiwango cha Juu, ambapo Miezi hiyo mitatu ni ya Ngongeza ya muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika. 
Sehemu ya Muonekano wa mbele wa jengo
Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, Tayari Ukaguzi wa Mamlaka za Jiji na Usalama Wa Majengo Umeshakamilika na Ruhusa ya Matumizi kutolewa. Tayari jengo hilo limeshapata Wapangaji Watatu Ambao wapo kwenye Jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku Asilimia 21 ya Wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na Wapangaji Wengine 24 Wakiwa katika Mazungumzo.

Aidha kwa Maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi Za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili Jipya, huku mkakati wa PPF Ukiwa ni kuhakikisha Baada ya Mwaka mmoja Jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji Maeneo yote kwa shughuli za ofisi na Biashara. 
Mkandarasi Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na Wakandarasi Wengine kwa Huduma za Jengo kama vile ICT na Usalama – SSTL Group Ltd, Lifti – S.E.C (EA) Ltd, AC – M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji taka – Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International Ltd. Pia kulikuwa na Mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama makazini OSHA, Idara ya maji Asurha – AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB. 
Injinia Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia Meneja wa jengo hilo kutoka PPF Bw..
Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha (kulia) akishuhudia makabidhiano rasmi ya jengo jipya la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo
Meneja wa PPF Uwekezaji Bw Selestine Some (kushoto) akimkabidhi ufungua kama ishara ya kuhamishia usimamizi wa jengo la PPF Plaza kwa Menenja Rasilimali, Bw Selemani Kituli wa PPF Kanda ya Kaskazini


Zawadi Dotto Aibuka Mshindi Wa Mashindano Ya Ulimbwende Ya MissAlbinism 2016

Na Mwandishi Wetu

New PictureMrimbwende Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.
Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.
Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.
New Picture (1)

No comments:

Post a Comment