Sunday, 7 February 2016

DC Paul Makonda Atoa Siku 20 Wenyeviti Wote Wa Serikali Za Mitaa Kinondoni Jijini Dar es salaam Wapewa Ramani Za Mitaa Yao

New PictureMkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
New Picture (1)Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani

Na Kalonga Kasati

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.
Makonda amewataka Watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea Haki wananchi katika kumaliza Migogoro ya ardhi.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Alisema Migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa Ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa yakiongeza matatizo.
“Leo tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa nawaagiza kuanzia sasa Mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,”alisema.

Alisema watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi.
“Kibaya zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,”alisema.
Aliongeza kuwa “Sina hofu wala uoga wala sina sifa ya kupendwa wala kutafuta kupendwa hivyo Uitahakikisha ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya migogoro hii ya ardhi Kinondoni na kuwa historia na nikitaka jambo huwa sishindwi”alisema.

Alisema baada ya wenyeviti hao kupewa ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilium Lukuvi na maofisa wa ardhi.
“Hapo sasa watakaobainika kuhusika katika michezo michafu na kuchochea migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke nao maana wameshindwa kazi”alisema

Makonda aliwataka wenyeviti hao kuonesha maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa ili kuchukua Hatua kwani wenye dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa wanateseka na migogoro hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Juliana Letara alisema Wenyeviti wote watapewa ramani za mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini hivyo atawapatia ramani hizo.

Alisema kutokana na migogoro mingi ya ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa kuwa kesi zote za mabaraza ya kata zinaigharimu serikali zaidi ya milioni tatu kwa siku.

Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila
“Tulikopa benki ya TIB mkopo kwa ajili ya kupima Viwanja likiwemo eneo la Mabwepande lakini kila siku tunatozwa riba ya sh.milioni tatu jambo ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana na ndio maana tunauza Kiwanja hadi milioni 20 na 30,”alisema.

Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambao walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu katika Manispaa hiyo likiwemo la maofisa mipango miji.

Alisema wako tayari kufanyazi na Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo cha ardhi kwa kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.

Rose Muhando naye amafuata Mwaitege Tamasha la Pasaka

Na Mwandishi Wetu
 
Image result for rose muhando
 
MWIMBAJI Guli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Rose Muhando amekuwa wa pili kuthibitisha kushiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama Muhando Ameungana na mwenzake Bonny Mwaitege ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha katika tamasha hilo.
Msama alisema tamasha hilo mwaka huu linatarajia kufanyika Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28) ambako alitoa wito kutoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.
Aidha Msama alisema dhamira ya Tamasha la Pasaka ni wenye uhitaji maalum ambao ni yatima, walemavu na wajane.
Msama Alisema sababu ya kupeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa ni kufikisha Ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo sambamba na kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’
.
“Tunalipeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa kwa sababu ya kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo ambayo miaka iliyopita iligubikwa na mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’,” alisema Msama.

No comments:

Post a Comment