Makamishna ZEC wapinga kurudiwa uchaguzi Zanzibar
Makamishna wa ZEC Wakipinga kurudiwa Uchaguzi wa Zanzibar wakati Wakiongea na Wanahabari leo Jijini Dar.
Na kalonga kasati
Wakati wadau mbalimbali wa Masuala ya kisiasa Wakipinga kile
kinachoendelea visiwani Zanzibar, nao Makamishna Wawili wa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Ndugu NASSOR KHAMIS MOHAMED Na AYOUB HAMAD Wameibuika Jijini Dar es salaam leo na kupinga Marudio ya Uchaguzi Unaotarajiwa kufanyika Mwishoni Mwa Mwezi huu kwa Madai kuwa Uchaguzi
huo sio Halali kulingana na Matukio Yaliyotokea Tangu kufanyika kwa Uchaguzi Halali wa Oktoba 25 Mwaka Jana.Wakizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam Makamishna hao Wamesema kuwa Sababu kubwa ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo ni kutokana na kuvurugwa kwa katiba ya Zanzibar Tangu tukio la kufutwa kwa Matokeo ya Uchaguzi wa Mwaka Jana ambapo Wamesema kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Hakuwa na Mamlaka ya kisheria kufuta uchaguzi huo Bila kuwashirikisha Makamishna wa Tume hiyo.
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar NASSOR KHAMIS MOHAMED Akizngumza na Wanahabari (hawapo pichani) Mapema leo jijini Dar es Salaam.
Wameongeza kurudiwa kwa uchaguzi huo ambao unatarajiwa kutumia zaidi ya bilioni saba hadi kukamilika kwake ni Matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwani uchaguzi Zanzibar ulishafanyika na tayari na kinachoendelea ni mbinu za kuubatilisha uchaguzi huo.
Wameongeza kuwa Tukio la kufutwa kwa uchaguzi huo lilitanguliwa na matukio kadhaa ambayo yalionyesha Wazi kuwa kuna kikundi cha watu ambacho kinamshauri Mwenyekiti wa Tume hiyo JECHA SALUM JECHA na sio maamuzi ya tume nzima.
Mjumbe Mwingine AYOUB HAMAD akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu kile kinachoendelea Zanzibar.
Ameendelea kusema kuwa Baada ya Maamuzi ya Tume ndipo siku iliyofuata Mwenyekiti JECHA hakufika katika ujumuishaji wa Matokeo kwa siku nzima na ndipo waliposikia kuwa Ametangaza kufuta Uchaguzi bila kuwashirikisha Wajumbe wengine wa tume hiyo na baada ya hapo ndipo ofisi yetu ilianza kuzungukwa na Wanajeshi na kuamuriwa tusifanye lolote huku jaji mkuu wa Mahakama ya Zanzibar naye akiwa Amekamatwa na kupekwa polisi.
Wamesema kuwa kwa matukio kama hayo wanaamini kuwa tume hiyo imeacha kufanya kazi zake kisheria Na sasa inafanya kazi kisiasa jambo ambalo linampotezea sifa mwenyekiti wa ZEC kuendelea kuiongoza Tume hiyo.
Aidha wamesema kuwa hali iliyopo ndani ya tume kwa sasa sio hali ya kawaidia ambayo inaweza kusimamia Uchaguzi wa haki kwani wajumbe wamekuwa wakipingana kwa kila hoja inayoletwa jambo ambalo linafanya uchaguzi wa marudio kutiliwa mashaka na wajumbe wengi wa tume hiyo.
Wajumbe hao wa ZEC wametoa wito kwa wajumbe wengine ndani ya tume hiyo kuacha kufuata mkumbo na kuamua kusimamia sheria inavyosema ili kuwapatia wazanzibar haki yao ya kikatiba
No comments:
Post a Comment