Thursday, 4 February 2016


Bondia Mada Maugo kushoto akipokea sehemu ya malipo ya awali kutoka kwa mratibu  Rajabu Mhamila ‘Super D’ wa mpambano wake na Abdallaha Pazi. utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka.

Na Mwandishi Wetu
Mabondia Mada Maugo na Abdalla Pazi ‘Dulla Mbabe’ wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa   taifa mpambano wa raundi nane KG 76.
akizungumza wakati wa kutiliana saini mikataba hiyo kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ambaye ni mratibu wa mpambano uho
amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo ambao wanatamba katika tasnia ya masumbwi nchini
ili wapenzi wa mchezo wa masubwi waburudike siku hiyo ya sikukuu ya pasaka
mbali na mpambano uho siku hiyo bondia chipkizi anaekuja kwa kasi zaidi katika mchezo wa masumbwi Vicent Mbilinyi anaetokea katika Super D  Boxing Promotion atakae pambana na Mwinyi Mzengela mpambano wa KG 63 raundi nane mpambano mwingine utawakutanisha bondia Cosmas Cheka na Mohamed Matumla na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali

Jaji Mutungi Asajili Cama Kipya Cha Siasa

indexNa. Kalonga kasati
VYAMA vya Siasa nchini vimeaswa kuepukana na migogoro na kutumia vikao vyao katika kuendeleza shughuli zao za kisiasa.
Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis Mutungi wakati akikabidhi Cheti cha Usajili wa muda kwa Chama kipya cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA).

Aidha, Jaji Mutungi amevitaka Vyama vya siasa nchini kufanya siasa na sio uanaharakati kwaki kwa kufanya hivyo malengo yao yatatimia na kuifanya Tanzania kuwa na amani.
‘’Msipende kukimbilia kwenye vyombo vya habari mnapokuwa na migogoro bali malizeni tofauti zenu ndani ya vikao vyenu kulingana na Katiba ya Vyama vyenu’’, alisema Jaji Mutungi.
Aliongeza kuwa, Tanzania inapaswa kuwa na vyama vya siasa vinavyojitambua na vinavyojua wajibu wao katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani siasa sio chuki wala uasama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) Bwana Laban Nkembo amesema kuwa, chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuiweka Tanzania kimaadili na uwajibikaji kwa kuwa kinabeba mambo makubwa mawili yakiwemo Amani na Upendo.

Ameongeza kuwa, chama chao sio cha Upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani Hivyo, kinaahidi kushirikiana na Chama Tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho.
‘’Chama chetu sio cha upinzani, tunataka nchi nyingine duniani ziwe zinakuja kujifunza Tanzania kuhusu amani na maendeleo tulionayo’’, alisema Nkembo.

Aidha, amebainisha kuwa, chama chao cha CM-TANZANIA kitatoa ajira za kudumu kwa Wanachama wake na hata kwa wale wasiokuwa wanachama ambapo kimeshaandaa Idara ya usimamizi mzuri wa huduma kwa jamii kama vile Wazee, Wajane, Walemavu pamoja na Yatima.
CM-TANZANIA ni Chama cha 23 kupokea usajili baada ya Vyama vingine vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.

waajiri waaswa kutouza fomu za opras kwa watumishi

NEMBO YA TAIFA
Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewataka  waajiri wote nchini kuhakikisha watumishi  wao wanapata Fomu ya wazi ya Mapitio na Upimaji Utendaji Kazi( OPRAS) wa utekelezaji bila usumbufu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo cha mawasiliano cha Ofisi hiyo imeeleza kuwa, kuna baadhi  ya Taasisi za Umma watumishi wanaelekezwa kununua fomu za OPRAS kutoka kwa watu binafsi, kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.
Fomu za OPRAS haziuzwi hivyo watumishi hawatakiwi kuzinunua, endapo mtumishi atashawishiwa au kulazimishwa kununua fomu hizi atoe taarifa Dawati la Malalamiko Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora ili hatua stahiki zichukuliwe, imefafanua taarifa hiyo.

Pia Fomu hizo zinapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-Menejiment ya Utumishi wa Umma yenye anwani ya www.utumishi.go.tz, hivyo waajiri wanaelezwa kutembelea tovuti hiyo.
Aidha, Serikali ilianzisha matumizi ya mfumo wa wazi wa mapitio na Tathimini ya Utendaji Kazi OPRAS mwezi Julai mwaka 2004 kupitia waraka wa Utumishi Na.2 wa mwaka 2004 na kufuta mfumo wa zamani wa kupima utendaji kazi wa mtumishi kwa njia ya siri.

Mabadiliko ya kutathimini UtendajI kazi wa Watumishi wa Umma kwa uwazi yanakwenda sambamba na Sera ya Menejiment na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa mwaka 2008 na kusisitiza uwekaji wa mifumo ya Menejimenti ya utendaji bora wa kazi inayojali matokeo.

No comments:

Post a Comment