Tuesday, 9 February 2016

Asilimia 10 Ya Watanzania Wanamiliki Uchumi Wa nchi

uw1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw4 uw5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia  au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
uw7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa  Wadau wa Uwezeshaji Wananchi  Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw8
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola   (wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. 

Na Kalonga Kasati
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi. 
“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake  na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.

Mbunifu Wa Mavazi Amina Design Atoa Mada Kuhusu Faida Za Ujasiliamali  Kwa Wanawake Wa Zanzibar

Mbunifu wa Mavazi Amina  Plummer Akitoa Mada kwenye Semiana ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Zanzibar yenye Lengo la Kuwafundisha Mbinu Mbalimbali za Biashara pamoja na Matumizi Sahihi ya Vipodozi Pendwa vya Luvtouch.
Mbunifu wa mavazi Amina Plummer amewaasa wanawake wa zanzibar kujikita kwenye ujasiriamali kwa kuwa ndio njia pekee ya kumkomboa mwanamke.amesema ajira nyingi zimekuwa na ubaguzi na pili ni nafasi chache sana zinatolewa kwa wanawake hivyo basi wanawake hawana budi kujikomboa kwa njia ya ujasiriamali.mama amina alisema hayo wakati akitoa mada alipowatembelea wanawake wa zanzibar walioniufaika na mradi wa manjano dream makers ulio chini ya taasisi ya manjano foundation yaliomalizika kwenye hotel ya mtoni marine zanzibar.
Mbunifu wa mavazi Amina Design akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Pamoja wa Baadhi ya wasaidizi Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation.
Akieleza Zaidi Mama Amina Plummer Ambaye  ni Mbunifu wa Mavazi amewaomba wanawake wa Zanzibar Kupenda Ujasiriamali kwa Kuwa ni Kazi Pekee ambayo kadiri Unavyoifanya kwa Juhudi na Maarifa Pia  inasaidia Kuongezeka kwa Kipato cahako.Hivyo wakina mama wa Zanzibar hawana Budi Kuchangamkia nafasi hiyo ya kujifunza Ujasiriamali Kutoka Taasisi Ya Manjano Foundation .
Washiriki wa Semina Hiyo kutoka  Visiwani Zanzibar wakisikiliza kwa Makini Mada zilizokuwa zikitolewa kwenye Mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment