
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira, imewataja wafungwa walio kwenye msamaha huo ni wale wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua Kikuu na Saratani walio katika terminal stage, wazee wenye umri wa miaka 70 u zaidi ambao umri wao umethibitishwa na jopo la madaktari chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa ama wilaya.
Wengine walionufaika na msamaha huo ni wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani ama walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya, pamoja na wafungwa walemavu wa mwili na akili, ambao ulemavu wao umethibitishwa na jopo la madaktari.
Hata hivyo msamaha huo ambao umetolewa kwa mujibu wa madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, msamaha huo hauwahusu wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na wale waliohukumiwa kifungo cha maisha pamoja na wale wanaotumikia kifungo kwa makosa ya rushwa, unyang’anyi wa kutumia silaha, mashambulio ya kunajisi, kubaka na kuwapa mimba wanafunzi.
No comments:
Post a Comment