Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (BLM), Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein, kesho tarehe 15/12/2016 anatarajia kukiongoza Kikao cha
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo
vya habari iliyotolewa leo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar –
Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Waride Bakar Jabu, amesema kikao hicho
cha kawaida cha siku moja kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui
kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Amesema kikao pamoja na mambo
mengine, kitapokea na kujadili Mapendekezo ya wanachama wa CCM wanaoomba
kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Dimani na kuongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Aidha, Katibu Waride amesema kikao
hicho kilitanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,
kilichokutana tarehe 14 Novemba, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, kwa lengo la
kuandaa Agenda za kikao hicho.
“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”
Waride Bakar Jabu
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
Idara ya Itikadi na Uenezi – CCM
ZANZIBAR.
14/12/2016
No comments:
Post a Comment