
Mabao ya kipindi cha pili ya Bryan Heynen na Leandro Trossard yalitosha kuipa ushindi miamba hiyo ya Ubelgiji na kusonga mbele katika hatua ya mtoano.
Kikosi hicho ambacho pia kina nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kinasonga mbele katika hatua ya mtoano wa mashindano hayo ya Ulaya kwa kumaliza kileleni mwa kundi lake.
Licha ya Samatta (Pichani chini) kuanza katika mchezo huo, alishindwa kuongeza bao katika hazina yake ya mabao tangu alipojiunga na miamba hiyo Januari mwaka huu.
Hadi sasa, Samatta ameweka kimiani mabao 13 katika mashindano yote tangu alipojiunga na miamba hiyo ya soka Ubelgiji.
Ushindi huo wa jana mchana ugenini kwenye Uwanja wa Citta del Tricolore, umewafanya Genk kumaliza hatua ya makundi wakiwa kileleni mwa msimamo wa kundi lao na kusubiri ratiba ya hatua ya mtoano ya timu 32.
Genk imemaliza michezo yao sita ikiibuka na ushindi katika mechi nne na kufungwa miwili, ikifunga mabao 13 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tisa huku ikijikusanyia pointi 12.
Timu hiyo imefuzu kutoka Kundi F pamoja na Atletico Bilbao iliyomaliza katika nafasi ya pili kwa pointi 10, huku wakiziacha Rapid Wien na Sassuolo ya Italia.
No comments:
Post a Comment