Jose Mourinho amekataa Kusaini Mkataba na Man U
Wakati Wapenzi wa Manchester United
wakiwa na shauku kubwa kumpokea Kocha mwenye Vituko vingi uwanjani kutua
Timu hiyo ya Jiji la Manchester Jose Mourinho linaonekana kuota Mbawa.
Mourinho amekana habari zote zinazo
muhusu yeye kuwa hana mkataba wowote wa kuifundisha timu hiyo msimu ujao
na kwamba waachene na habari hizo, pia amewaambiwa kuwa Van Gal ni
rafiki yake walikuwa wote miaka michache iliyo pita kwa hivo hawezi
kuchukua mkataba.
TETESI
Siku kadhaa zilizo pita kulikuwa na
tetesi kuwa kocha huyo amesha chukua mkataba wa Awali(Pre-Contract) kwa
ajili ya kuifundisha Manchester United wakati huo huo kulikuwa na Taarifa kuwa Luois Van Gaal imetaarifiwa kuwa atakuwepo msimu ujao na
pesa za usajili Amepewa.
MTAZAMO
Jose Mourinho mara nyingi hupenda
kucheza na akili za watu huenda ameshachukua mkataba lakini kwa kuona
thamani na utu wa Van Gaal ambae aliwahi kuwa chini yake hataki
aonekane ana fitna ndio maana anaficha ukweli, vile vile vyombo mbali
mbali viliwahi kutoa Habari kuwa huenda Van Gaal aka staafu baada ya
msimu huu kuisha hii pia inatupa Matumaini kuwa Jose Mourinho anacheza
na hakili za watu yeye ndiye kocha msimu ujao.
HISTORIA
Jose Mourinho (JM) amepata umaarufu
alipo ichukua Fc Porto ya Nchini kwake Ureno na kuchukua ubingwa wa Ligi
hiyo pamoja na UEFA kama ilivyo kawaida yake akipata mafanikio Msimu
unao fuata anaondoka baada ya uwekezaji wa Roman Abromovic 2004-2005
katika Timu ya Chelsea akamsogeza Stanford Bridge kukinoa kikosi hiko
akachukua ubingwa mara Mbili wa Epl akatimkia Inter Milan huko nako
akachukua UEFA akiwa na Samuel Et’oo Baada ya mafanikio aka enda Real
Madrid nako kachukua La liga msimu mmoja karudi Chelsea akarudia tena
kwa sasa hana timu.
No comments:
Post a Comment