Chelsea Vs Man City Leo

Unaambiwa
asiyefanya kazi na asile lakini hapa ni kinyume mchezaji analipwa
mshahara ili Apumzike. Kuyaelewa maneno yangu inahitajika hekima na
busara kubwa sana na kama Wewe ni mtu wa soka utakuwa umeanza kuhisi
nazungumzia nini, ni ile tofauti ya soka la Ulaya na Bongo.
Manchester city wamecheza mashindano ya
kimataifa siku ya Jumanne lakini leo wanashuka Dimbani kucheza mchezo wa
ligi kuu dhidi ya Chelsea majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika
mashariki, lakini ingekuwa hapa kwetu lazima timu ingeomba kupumzika
kutokana na Kisingizio cha wachezaji kuchoka ama hakika tutabaki hapa
hapa na ujanja ujanja wetu usio Na tija kwenye soka.
Mechi kubwa leo Epl
Chelsea
John Terry, Eden Hazard na Loic Remy watakosa mechi ya leo dhidi ya Man
City kwasababu Bado ni majeruhi, lakini Nemanja Matic na Gary Cahill
wamepona na wapo fiti kuisadiaklabu Yao kusaka alama tatu mhimu.
Man City
Vincent Kompany ataikosa mechi hiyo kwa kwa sababu ya majeraha yake ya
misuli lakini Anaweza kurejea Jumanne. Raheem Sterling amerudi mazoezini
baada ya kusumbuliwa na Majeraha japo bado hawezi kuwa tayari kwa
mchezo wa leo.
Kocha wa Chelsea
Guus Hiddink hajawahi kupoteza mechi mfululizo kama meneja tangu 2004
akiwa PSV Eindhoven na ameweza kuisaidia Chelsea kutopoteza michezo 15
hadi ilipokutana na Swansea Na kupoteza. Hiddink hajawahi kupoteza mechi
akiwa darajani katika vipindi viwili alivyoinoa klabu hiyo ameshinda 6
na Sare 7.
Kocha wa Man City
Manchester City hawajapoteza mechi za ugenini tangu Oktoba. Kikosi hicho
cha Manuel Pellegrini kimepoteza mechi moja tu katika mechi saba za
mwisho walizocheza ugenini wakishinda 3, sare 3 na wamefungwa 1.
Mchezaji Anayefanya vizuri
Kevin De Bruyne akiwa kwenye kiwango kizuri msimu huu hadi sasa amefunga mabao 15 na kusaidia Mengine 12.
No comments:
Post a Comment