Tuesday, 19 April 2016

Harmonize: Ofisini Kwetu WCB Sinza, Kuna Mahitaji yote Muhimu kwa Binadamu.


Harmonize: Ofisini kwetu WCB Sinza, kuna mahitaji yote muhimu kwa Binadamu.

 Na Mwamvita Mtanda

Msanii wa kizazi kipya aliyechini ya lebo kubwa ya muziki Tanzania WCB, Harmonize, Amesema ofisi yao ya Wasafi iliyopo Sinza ina kila kitu ambacho Huweza kumfanya hata Akashinda wiki nzima kwenye studio hiyo.

Akizungumza na Mwandishi Wetu , Msanii huyo ameweka Wazi kuwa Makazi yake ni Tegeta lakini muda mwingi anautumia kikazi Sinza.

“Mi Naishi state House Tegeta, ila muda mwingi tunakuwa ofisini na bosi kwa Sababu ni Nyumba kubwa kuna kila kitu, kuna Vyumba vya kulala, Gym, kila kitu so kuna muda Tunakaa Sinza siku Mbili hadi tatu tuko Sinza tu, sababu ofisi kubwa ina sehemu nyingi za kupumzika” Alisema.

No comments:

Post a Comment