AZAM FC Kuendeleza Ushindi Leo Tunisia
Na Kalonga Kasati
AZAM leo ipo Tunis, Tunisia kumenyana
na Esperance ya huko katika mechi ya marudiano ya Raundi ya pili ya
michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wawakilishi hao wanahitaji ushindi au
sare ya aina yoyote kusonga mbele kwenye michuano Hiyo baada ya kushinda
mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam
Complex, Chamazi Dar es Salaam.

Mechi
hiyo ya leo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Olympique de Rades
mjini Tunis Na kocha wa timu hiyo Stewart Hall alisema timu yake iko
vizuri kwa mechi hiyo.
“Timu iko vizuri, tunatarajia mchezo
utakuwa mgumu hasa kwa vile tumeshinda mechi ya kwanza nyumbani hivyo
tumejiandaa na kila mmoja anafahamu wajibu wake”.
Kocha Hall alifafanua kuwa wanacheza na timu bora Afrika, hivyo uwezekano mkubwa wa Wapinzani wao kubadilika kwao ni mkubwa.
“Timu kubwa hizi zina mbinu nyingi
kwenye mechi, unaweza kuwakuta wamebadilika kabisa Mechi ijayo, lakini
yote hayo tumejipanga kukabiliana nayo,” alisema.
Ikiiondosha Esperance kwenye mechi
hiyo, Azam itaingia hatua ya 16 bora ambapo itacheza na Timu itakayotoka
kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kufuzu hatua ya makundi, Endapo itashinda.
Pambano hilo la Azam FC linatarajia kuanza saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni
kati ya Stade Gabesien itakayocheza na Zanaco, Sagrada Esperanca dhidi
ya Vita Club Mokanda, Medeama na El Ahly Shandy, SC Villa itacheza na
Fath Union Sport, Misr Makkassa itacheza na CS Constantinois, Enppi
itacheza na Mounana Na Kawkab Marrakech itamenyana na Mouloudia Club
D’oran.
No comments:
Post a Comment