Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akikabidhiwa magari ya
kubebea wagonjwa(Ambulance) 10 kutoka kwa balozi wa Qatar nchini
Tanzania Bw. Abdullaral Suwaid kushoto wakati wa makabidhiano hayo
yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Na Ally Daud –MAELEZO
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto wamejidhatiti kutatua changamoto
zinazoikumba sekta za afya nchini ili kutengeneza Taifa lenye wananchi
imara kwa maendeleo ya jamii na uchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa
ufunguzi wa mkutano mkuu wa kutathimini nakurekebisha Sera ya Afya
uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
“Katika mkutano huu tumeadhimia
kuongeza bajeti ya dawa nchini kutoka milioni 31 mpaka kufikia milioni
231 ambazo zitachangia kuondoa uhaba ambao umejitogeza hivi
karibuni”Alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
katika mkutano huo wanatarajia kupata njia za kutatua changamoto
mbalimbali zinazoikumba Sekta ya afya nchini.
Kwa Mujibu wa Waziri Ummy amesema
kuwa sekta ya Afya inaupungufu wa watumishi kwa asilimia 49 hivyo
kunauhitaji mkubwa wa watumishi katika sekta hiyo ambapo watahitajika
ili kuimarisha huduma bora.
Amesema kuwa lengo la mkutano huo
ni kupata kinga juu ya magonjwa ya sioambukizwa ikiwemo kisukari,
Magonjwa ya moyo na shinikizo la damu ambapo watazindua kampeni ya
mazoezi ya viungo Desema 17 mwaka huu Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake Naibu Waziri
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo
amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha zahanati zote za serikali zinatumia
mashine za Kieletroniki katika kukusanya mapato ya sekta za afya ili
kuboresha Huduma.
Wakati huo huo na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipokea msaada
wa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) 10 kwa ajili ya hospitali
zaTanzania kutoka ubalozi wa Qatar nchini.
Akipokea magari hayo Waziri Ummy
amesema kuwa magari hayo yatasambazwa katika hospitali za rufaa
ilikusaidia kupunguza idadi ya vifo vya wagonjwa wanaocheleweshwa
kutokana na kukosa usafiri wakuwahishwa kwenye hospitali nyingine.
Aidha Waziri ummy alibainisha
hospitali zitakazopata magari hayo ni Mombotanga, Benjamini Mkapa Mbeya,
Taasisi ya Jakaya kikwete Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Mikoa ya
Dodoma na Ruvuma, hospitali ya Kigamboni na NzegaTabora.
No comments:
Post a Comment