Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya
Haki za Binadamu na Wananchi pamoja na Watumishi wa Kituo cha Huduma za
Sheria, mjini Unguja, Zanzibar (hawapo pichani). Masauni katika hotuba
yake, alisema matukio ya unyanyasi yanaongezeka kwa wingi nchini, hivyo
amewataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji
katika vyombo husika kwa wakati. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kituo cha
Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter na kulia ni
Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji Mpatani.
Wananchi wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa
anatoa hotuba yake katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu katika
Kituo cha Huduma za Sheria, mjini Unguja, Zanzibar. katika hotuba yake,
Masauni aliwataka wananchi nchini, kutoa taarifa za ukatili na
unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa
Baraza la Vijana Zanzibar, Khamis Rashid Kheri baada ya kupokea
Matembezi ya kupinga Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto yalioandaliwa
na Baraza hilo, Mnarani Mwembe Kisonge, mjini Unguja, Zanzibar. Wapili
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas.
Sehemu ya vijana ambao walishiriki
Matembezi ya Kupinga Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto wakiwa wameshika
bango ambalo lina ujumbe unaowataka askari kuwasaidia wananchi zaidi
katika mapambano ya kudhibiti matukio ya unyanyasaji nchini. Vijana hao
walipokelewa na mgeni rasmi katika tukio hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Mwenyekiti wa Kituo
cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter (wapili
kushoto waliokaa), Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji
Mpatani (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na
Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani. Masauni
alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa ZLSC, mjini Unguja, Zanzibar.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment