Wananchi wakiangalia daladala lenye namba za usajili T 161 CRP
lililoacha njia na kupinduka Mbagala Misheni kwa Bluda Dar es Salaam leo
asubuhi na kujeruhi watu watatu.
Watu watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya daladala walikuwa wamepanda
kutoka Temeke kwenda Mbagala Kuu kuacha njia na kupinduka jijini Dar es
Salaam.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi wa Temeke
ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa polisi alisema
ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 na nusu asubuhi.
Alisema daladala hilo liliacha njia na kutumbukia kwenye mtaro eneo la
Mbagala Misheni kwa Bluda baada ya kuteleza kutokana na mvua zilizokuwa
zikinyesha.
Alisema baada ya ajali hiyo wananchi walifika kutoa msaada kwa majeruhi ambao walikimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.
Alitaja daladala hilo kuwa ni lenye namba za usajili T 161 CRP ambapo
alitoa mwito kwa madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari yao hasa
katika kipindi ambacho mvua zinanyesha.
No comments:
Post a Comment