Mchezaji kandanda wa umri wa miaka 81, anayeaminika kuwa mchezaji soka mkongwe zaidi nchini Uingereza, anatafuta klabu mpya.
| Dickie Borthwick alianza kucheza soka mwaka 1947 akiwa na miaka 12 |
Dickie Borthwick, anayetoka Weymouth, Dorset, alianza kucheza kandanda mwaka 1947 akiwa na miaka 12.
Alikuwa mchezaji katika klabu ya wanajeshi wastaafu ya Wyke kabla ya
klabu hiyo kuvunjwa. Hata hivyo, anakiri kwamba huenda umri umemzidi na
haitamfaa kucheza kwenye ligi ya wanajeshi wastaafu tena.
ALiambia gazeti la The Mirror nchini Uingereza kwamba amepokea mwaliko
wa kujiunga na klabu ya soka ya matembezi lakini amesema anataka
kushiriki soka yenye kasi kiasi.
| Mr Borthwick anasema amefunga zaidi ya magoli 400 katika miaka 69 aliyocheza kandanda |
Mr Borthwick anasema amefunga zaidi ya magoli 400 katika miaka 69 aliyocheza kandanda
Bw Borthwick, ambaye alitibiwa saratani ya tezi dume miaka mitatu
iliyopita, anasema bado yuko sawa kiakili na kimwili na bado anaweza
kukimbia na kusakata gozi.
Anasema anatumai wachezaji wa klabu ya soka yakutembea, ambayo imempa
mwaliko, wanaweza kufanya mazoezi na labda waongeze kasi kwenye mchezo
wao.
Amesema yuko tayari kujiunga na klabu yoyote ya wazee wa zaidi ya miaka 60 eneo la Dorset.
Anasema amefunga mabao 400 katika miaka 69 aliyocheza soka na hajawahi
kuadhibiwa mchezoni katika mechi zote rasmi 1,600 ambazo amewahi
kucheza.
No comments:
Post a Comment