
Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amefanya mabadiliko makubwa kutoka kikosi kilichlambwa 2-1 na Mbeya City katikati ya wiki, leo akiwaanzisha pamoja washambuliaji wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe, Mzambia Obrey Chirwa na Mzimbabwe Donald Ngoma.
Na ajabu zaidi leo ni kwamba, Pluijm amemuanzisha kinda Yussuf Mhilu wakati Juma Mahadhi na kipa aliyesimama langoni dhidi ya Mbeya City akitunguliwa mabao mawili ya mashuti ya mbali, Deo Munishi 'Dida' hata benchi hawapo. Hassan Kessy ameanzishiwa benchi na beki ya kulia leo ameanza Mbuyu Twite na langoni yupo Benno Kakolanya.
Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Benno Kakolanya, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Yussuf Mhilu, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Deus Kaseke.
Katike benchi wapo Ally Mustafa 'Barthez', Oscar Joshua, Matheo Anthony, Hassan Kessy, Vincent Andrew, Amissi Tambwe na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro
No comments:
Post a Comment