Friday 25 November 2016

Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Ndugu Slyvester M. Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  kuanzia tarehe 17 Novemba, 2016.
Aidha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania;
  1. Bw. Valerie Ndeneingo Sia Masoka, Communications and Advocacy Specialist, Dar es Salaam,
  1. Dkt. Jabir Kuwe Bakari, Mtendaji Mkuu, Wakala wa Serikali Mtandao, Dar es Salaam,
  1. Bi. Butamo Kasuka Philip, Managing Partner, Top Attorneys, Dar es Salaam, na
  1. Dkt. Mzee Suleiman Mndewa, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Zanzibar.
Uteuzi wa wajumbe hao ni kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Na. 12 ya Mwaka 2003. Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
Imetolewa na:
Prof. Faustin Kamuzora
KATIBU MKUU – MAWASILIANO

No comments:

Post a Comment