Saturday 26 November 2016

Rais wa Zamani wa Cuba, Fidel Castro Afariki Dunia

CUBA: Rais wa zamani wa Cuba, na kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha nchini humo, Fidel Alejandro Castro Ruz amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 90.
Kifo cha Castro kimetangazwa kwenye Televisheni ya Taifa na Rais wa sasa wa nchi hiyo ambaye ni mdogo wa marehemu, Raul Castro.
Castro alichukua madaraka ya nchi hiyo baada ya kufanya mapinduzi mnamo mwaka 1959 na kuiongoza Cuba kwa miaka 49, kabla ya kuachia ngazi February 2008 na kumkabidhi uongozi mdogo wake, Raul Castro kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
Miaka miwili kabla, mdogo wake , Raul alishikila madaraka ya kaka yake wakati kaka yake alipofanyiwa upasuaji wa dharula wa utumbo mpana.
Baada ya Malkia Elizabeth II na Mfalme wa Thailand, kiongozi huyo wa Cuba ni wa tatu duniani kwa kukaa madarakani kwa muda murefu zaidi.
Wafuasi wake wamekuwa wakiamini kuwa, Castro ndiye aliyeirudisha Cuba kwa wananchi wake huku wapinzani wakipinga uongozi wake wa kimabavu.

No comments:

Post a Comment