Wednesday 23 November 2016

Mwinyi, Lukuvi wateta na JPM Ikulu

.



  



Rais John Pombe Magufuli,  amekutana na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Ikulu ambaye amempongeza kwa kazi kubwa aliyofanya katika kipindi cha mwaka mmoja aliokaa madarakani.
Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa Rais Magufuli pia amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi.
Baada ya mazungumzo hayo, Mwinyi amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli na kufanya nae mazungumzo kwa mara ya kwanza ni kumpongeza kwa kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani na pia kumpongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Mwinyi ameyataja baadhi ya maeneo ambayo Rais Magufuli ameyafanya kwa mafanikio makubwa kuwa ni mapambano dhidi ya rushwa na amebainisha kuwa hatua zilizochukuliwa katika kipindi cha mwaka mmoja zimedhihirisha kasi kubwa ya kukabiliana na tatizo hilo ikilinganishwa na wakati uliopita.

No comments:

Post a Comment