Tuesday 22 November 2016

Wachina Kupewa Elimu Ya Mlipa Kodi

 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Kwa mlipakodi (TRA), Richard Kayombo (kulia) akizungumza na wanahabari(hawapo pichani) pembeni yake Mchina ni Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina, Andrew Huang.

Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina, Andrew Huang akiongea jambo.

Mamlaka ya Tanzania (TRA) Kwa kushirikiana na Ubalozi wa China hapa nchini imeandaa semina Kwa ajili ya Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China kuhusu utoaji elimu juu ya kutambua mambo ya kodi na uwekezaji.
Akizungumza na Mwanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Kwa mlipa kodi, Richard Kayombo amesema kuwa elimu hiyo itakayotolewa ya mlipa kodi itahusisha namna ya kuzingatia na kuzitumia sheria za kutoza kodi sahihi na kukokotoa kodi ya zuio katika bidhaa na huduma na hivyo kuongeza ulipaji wa kodi Kwa hiari miongoni mwao.

Alifafanua kuwa katika semina hiyo kutakuwa na mada mbalimbali ikiwemo kutambua mabadiliko ya Bajeti 2016/17, masuala ya forodha,na uondoshaji wa bidhaa, kodi ya zuio hususani katika sekta ya ujenzi na kodi ya ajira ambapo wafanyabiashara hao watapata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi ili kuwawezesha kufanya shughuli zao Kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Aidha katika semina hiyo waziri wa viwanda na biashara anatarajiwa kufungua semina hiyo ambayo pia itahudhiriwa na Balozi wa China hapa nchini na zaidi ya wafanyabiashara 200 wa China wanatarajiwa kuhudhuria.

No comments:

Post a Comment