Friday 25 November 2016

Madee: Nyakati za Kikwete zilikuwa huru

Hitmaker wa Migulu Pande, Madee anammiss Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Muimbaji na rapper huyo anadai kuwa enzi za utawala wake, zilikuwa za uhuru ukilinganisha na sasa. Akiweka picha akiwa na Rais huyo mstaafu pamoja na wasanii wengine, Madee ameandika, “Zilikua nyakati huru sana.”
Kikwete anakumbukwa na wasanii wengine kwa jinsi alivyokuwa karibu nao ikiwa ni pamoja na kuwaita mara kwa mara kwa mazungumzo ikulu.

No comments:

Post a Comment