Saturday 26 November 2016

Maisha ya Fidel Castro enzi za uhai wake

 Picha za maisha ya Amri jeshi mkuu Fidel Castro,aliyeongoza mapinduzi ya kikomunisti na kuiongoza Cuba kwa miaka 50
Fidel Castro alizaliwa mwaka wa 1926, azaliwa mkoa wa kaskazini mashariki wa oriente nchini Cuba na tajiri wa ukuzaji wa miwa. Alijiunga na siasa za mapinduzi akiwa na umri mdogo

 Baada ya miaka miwili jela kwa kuongoza mapinduzi yaiyotibuka, alienda mafichono nchini Mexico. Mwaka 1956 alirudi na chama chake cha mapinduzi kikaongoza.Castro mwishowe akapata mamlaka ya kuiongoza Cuba tarehe 1,mwaka 1959,kama waziri mkuu kwa kumshinda Fulgencio Batista
 Mwaka 1961,Castrol aliongoza kikosi chake cha jeshi dhidi ya raia wa Cuba 1,500 waliokuwa uhamishoni. waliohamishwa walikuwa wanafadhiliwa na CIA, walivamia Bay of Pigs ili kuishinda serikali yake
 Alipata majaribio kubwa mwaka 1962 , pale rais wa Marekani John Kennedy alipomuonya kuondoa makombora yake kutoka cuba
 Mwishowe,viongozi Nikita Khrushchev na Castro waliondoa makombora na tishio la vita vya nyuklia vikazuiwa
 Amri jeshi mkuu huyo alipenda kushiriki mchezo wa baseball. Hapa anaonekana akicheza katika chuo cha ualimu huko Sierra Maestra mwaka wa 1962.
 Wacuba wengi walimchukulia kama dikteta wa ukandamizaji
 Mamia ya raia wa Cuba walikimbia makwao,kuelekea Marekani,kwa kutumia maboti yaliokuwa hatari
 Lakini Fidel Castrol alipata uungwaji mkono kuwa miongoni mwa viongozi waliohudumu kwa miaka mingi duniani
 Baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo, alimkabidhi rasmi madaraka ya urais kakake Raul.Alioneka mara chache,kabla ya kung’atuka madarakani mwezi Februari mwaka 2008
Mwezi Septemba, Fidel Castrol alihutubia umma kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne. Hotuba yake ilikuwa ya kwanza tangu mwezi Julai mwaka 2010 alipotoka kufanyiwa upasuaji wa utumbo. Alionekana kwa umma alipokuwa akisherehekea mwaka wa 90 wa kuzaliwa kwake mwezi Agosti

No comments:

Post a Comment