Wednesday 23 November 2016

Instagram yazindua video ya matangazo ya moja kwa moja

 Video ya matangazo ya moja kwa moja ya Instagram
Mtandao wa Instagram ndio mtandao wa huduma ya kijamii wa hivi karibuni kuzindua video za matangazo ya moja kwa moja.
Ukifuata nyayo za mtandao wa facebook,unaomiliki Instagram,You Tube pamoja na programu ya moja kwa moja ya Twitter ya Periscope ,Instagram imezindua programu mpya inayoruhusu wateja wake kuweka matangazo ya moja kwa moja wakati wowote.

Mtu yeyote anayetazama anaweza kutoa maoni yake kwa kuweka emoji ambazo hujitokeza katika video hiyo ya moja kwa moja.

 Instagram yazindua kanda za video ya moja kwa moja
Inaonekana kuwa ya kawaida,lakini kuna tofauti kubwa.Mara tu unapomaliza kuweka matangazo yako hupotea kabisa.
Hiyo inamaanisha hutaweza tena kusambaza link ya video yako kwa wanaotazama na hawataweza kuiona tena baada ya matangazo hayo.
Katika taarifa ,msemaji wa Instagram alisema kuwa hiyo inalenga kuwafanya wateja kuhisi faraja na kuweza kusambaza chochote wanachotaka kusambaza.

Instagram yazindua programu mpya
Programu hiyo itasambazwa kwa kundi la wateja wa mtandao huo kabla ya kutumika na kila mtu katika kipindi cha wiki chache zijazo.

No comments:

Post a Comment