Monday 28 November 2016

Mauzo soko la hisa Dar yaporomoka tena

Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ( DSE) yameendelea kushuka kwa wiki ya tatu mfululizo baada ya wiki iliyopita kuporomoka kwa asilimia 87.
Katika wiki hiyo iliyoishia Novemba 25, DSE imeeleza kuwa mauzo hayo yalishuka kutoka Sh4 bilioni hadi kufikia Sh500 milioni.
Kushuka huko kwa mauzo kulitokana na kuyumba kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa sokoni hapo kwa asilimia 85 kutoka hisa 671, 618 hadi 101, 809 wiki iliyopita.
Ripoti ya wiki ya mwenendo wa soko hilo iliyotolewa leo Jumatatu (Novemba 28, 2016) inaeleza kuwa kushuka huko kwa mauzo kunaweza kuhusianishwa na ongezeko la mauzo ya hati fungani zilizouzwa sokoni hapo wiki hiyo.

No comments:

Post a Comment