Thursday 24 November 2016

Timu ya KRC Genk kuwaalika Rapid Vien toka nchini Austria mchezo wa Europa League.

.images
Timu ya KRC Genk anayocheza mshambuliaji wa Tanzania Bwana Ally Samatta watakuwa kwenye uwanja wao wa Cristal Arena kuwaalika Rapid Vien toka nchini Austria mchezo wa Europa League.
Genk wanaongoza kundi F wakiwa na pointi 6 sawa na timu ya Atletico Club ya Hispania zikiwa na tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga na nafasi ya tatu inashikwa na Rapid Vien wakati Sassuolo nao wana pointi tano kwenye nafasi ya pili hivyo Genk wanahitaji kushinda ili kuweza kuweka matumaini ya kusonga mbele.
Wakina Samatta wataingia uwanjani kama nyuki kutokana mchezo uliopita waliweza kupoteza nchini Hispania kwa kufungwa magoli 5-3 dhidi ya Atletico club endapo watashinda watafikisha pointi 9 hivyo itabidi mchezo wa mwisho watacheza Italia Desemba 8 kucheza na Sassuolo.
Samatta amekuwa na bahati ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk kwenye michuano ya kimataifa tofauti na mechi za Ligi ya ndani na ikumbukwe kila kundi la Europa League hutoa timu mbili za juu ambazo huwazifuzu na kuenda kukutana na timu ambazo zimeweza kushika nafasi ya tatu kwenye michuano ya Champions League.

No comments:

Post a Comment