Sunday 27 November 2016

Bondia Shoga Adundwa Kwa Tko, Wenzake Wamshambulia Mitandaoni

 Bondia Orlando Cruz amekutana na kipigo kikali kutoka kwa Terry Flanagan ambaye alimuangusha na kushinda kwa TKO.
Cruz amekutana na kipigo hicho ikiwa ni mara ya kwanza tokea atangaze yeye ni shoga mwaka 2012 lakini bondia mwenzake amemshambulia hadharan
i.

 Peter Fury ambaye ni mmoja wa mabondia nyota na Frankie Gavin pia, wameandika kwenye mitandao ya kijamii wakieleza kipigo cha Cruz kinaonyesha tofauti ya mwanamke kamili, dhidi ya asiyekamilika.
Maneno ya mabondia hao wawili kupitia mtandao wa Twitter yanaonyesha kiasi gani walivyokerwa na uamuzi wa Cruz kujitangaza hadharani kwamba yeye ni shoga.
Wakati alipofanya hivyo, mabondia wengi walipinga wakionyesha wameingiliwa kwa kuwa inaonekana mchezo wa wanaume kamili, sasa wako ambao wameanza kufanya tabia hiyo mbaya na ya hovyo kabisa.

No comments:

Post a Comment