Tuesday 22 November 2016

RC Makonda: Wazazi Wenye Watoto Wahalifu ‘Panya Road’ Kukamatwa

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul, Makonda amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiingie katika matukio ya kihalifu.
Akizungumza leo Jumanne, Novemba 22 katika uzinduzi wa madarasa nane ya Shule ya Msingi Mbande iliyoko wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Makonda amesema mtoto yeyote aliye chini ya umri wa miaka 17 atakaye kamatwa kwa tuhuma za uhalifu, na wazazi wa mtoto huyo atakamatwa.
“Mtoto wa umri wa miaka 17 akikamatwa kwa kosa la uhalifu, uvamizi au akikamatwa kwa makosa ya uporaji au panya road nimewaambia polisi na wazazi wao akamatwe. Mtoto ni wakwako unatakiwa kuangalia muenendo wa mtoto wako, kwahiyo wazazi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao,” Makonda aliiwaambia wazazi pamoja na wanafunzi wa shule ya Mbande.

RC Makonda amewataka wazazi hao kuwahimiza watoto wao kusoma pamoja na kufuatilia maendeleo yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment