Monday 28 November 2016

Serikali kuweka Rada mpya kwenye viwanja vinne vya ndege.

Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho katika maandalizi ya kununua rada nne mpya zitakazowekwa kwenye viwanja vinne vya ndege vya Kilimanjaro,Mwanza,Mbeya na Julius Nyerere hili kuimalisha ulinzi wa viwanja vya ndege na anga la Tanzania na kuepuka utegemezi wa rada moja iliyopo hivi sasa.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Hamza Johari amesema hayo katika mkutano wa masuala ya usalama wa anga kati ya nchi na nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo amesema katika mpango huo rada ya uwanja wa Dar-es-Salaam inayotumika hvi sasa itabadilishwa kwakuwa ni ya muda mrefu.
Mkurugenzi wa miundombinu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Philipo Wambugu amesema ushirikiano kati ya nchi na nchi za Afrika Mashariki unazidi kukua na kuleta mafaniko ya kutosha.
Mshauri wa masuala ya kisiasa kwenye ubalozi wa China nchini Yang Tong amesema serikali ya China itaendelea kushikirikiana na nchi za Afrika katika masuala ya anga hili kufika malengo waliyojiwekea.

No comments:

Post a Comment