Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
kaikagua mashine ya MRI katika hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye Chuo
Kikuu cha Dodoma wakati Alipoitembela Aprili 9, 2016. Wapili kushoto ni
Naibu Waziri wa Afya, , Dkt. Hamis Kigangwala. (Picha na Ofisi ya Wziri
Mkuu.)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Khamis Kigangwala wakikagua mashine ya Mobile
Digital xray wakati walipotembelea hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye
Chuo Kikuu cha Dodoma Aprili 9, 2016. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Hospitali
hiyo Profesa Gesai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Taasisi Ya Kufundisha Lugha Ya “International Language Training Centre ” Yaboreshwa Zaidi Mazingira Ya Kujifunza.
Charles Mombeki ambae ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na Kimataifa Jijini Mwanza ya “International Language
Training Centre” akiwa amesimama katika jengo la taasisi hiyo iliyopo Isamilo (barabara ya Medical Research) Jijini Mwanza.
Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na Kimataifa Jijini Mwanza ya “International Language
Training Centre” akiwa amesimama katika jengo la taasisi hiyo iliyopo Isamilo (barabara ya Medical Research) Jijini Mwanza.
Mombeki
anasema taasisi hiyo imeboresha zaidi mazingira ya kujifusia ili
kukidhi mahitaji wasomaji. Pia anaongeza kwamba Taasisi hiyo imeboresha
mazingira kujifunzia kwa ajili ya Kituo chake cha Elimu ya Makuzi kwa
Watoto Wadogo (Day Care Centre) ambapo anawasihi wananchi kutembelea
taasisi hiyo ili kunufaika na fursa iliyopo hivi sasa kabla haijafikia
ukomo.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na
Kimataifa Jijini Mwanza ya “International Language Training Centre”
akitoa ufafanuzi kwa wanaohitaji kusoma katika taasisi yake. Pembeni ni
eneo rafiki kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya masomo au majadiliano
baada ya masomo.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na
Kimataifa Jijini Mwanza ya “International Language Training Centre”
akionyesha baadhi ya maeneo kwa ajili ya michezo ya watoto.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na
Kimataifa Jijini Mwanza ya “International Language Training Centre”
akionyesha baadhi ya maeneo kwa ajili ya michezo ya watoto.
Wasiliana na International Language Training Centre kwa nambari 0784 66 49 33 au 0754 66 49 33
Ili Usipitwe.
Waziri Ummy Mwalimu atembelea Hospitali za Mkoa wa Mbeya
Na Catherine Sungura, Mbeya
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mhe. Ummy Mwalimu
amefanya ziara katika hospitali zilizopo Mbeya na kuzitaka hospitali
zinazotumia mfumo wa ukusanyaji mapato wa kieletroniki wasibweteke na
mapato wanayoyakusanya kila siku.
Rai
hiyo imetolewa na aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee Na
Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya
kanda ya mjini Mbeya.
Ummy
alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa
katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa, vifaa na
vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi.
“Bado
tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia
ngazi zote, tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa,” alisema.
Aidha
alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa
itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma, hivyo Wameishauri Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa
hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji
wa dawa kwa haraka.
Waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia, kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa.
“Tunao
watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka
kwenye maduka ya dawa binafsi, hao hatutowafumbia macho na kuwapeleka
mahakamani”
Kuhusu
upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini, Waziri wa afya alisema,
nchi ina upungufu wa asilimia 52, hivyo serikali inatarajia kuajiri
watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa nchi
nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni.
Katika
hospitali ya uzazi ya Meta, waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi za
wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na
wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka
ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na
watoto njiti.
Hospitali
ya Kanda ya Rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi Milioni
mia tano na pia inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu
milioni mbili.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akisalimia na watumishi mara alipofika kwenye hospitali ya rufaa ya
mkoa ya Mbeya.
Waziri Ummy akimsalimia mtoto Jenifer Joel (9) mkazi wa Chunya aliyelazwa hospitalini hapo.
Waziri
wa afya akimjulia hali mtoto Baraka Jekonia (1) mkazi wa Chunya
aliyelazwa wodi ya watoto, Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kuwachaji
pesa wagonjwa wote wanaofika hospitali ya rufaa moja kwa moja bila
kupatiwa rufaa kutoka vituo vya afya vilivyopo jirani na wananchi ili
kupunguza msongamano kwenye hospitali za rufaa nchini.
Katika
hospitali ya uzazi ya Meta, Waziri Ummy Mwalimu alimsalimia Binti
Kanisia Komba aliyejifungua mtoto wa kike katika hospitali hiyo mama
wajawazito wote wanatibiwa kwa kadi ya bima ya afya inayodhaminiwa
mpango wa kusaidia akina mama wajawazito wa KFW toka Banki ya Ujerumani.
Hospitali
ya Meta tayari imetekeleza maagizo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ya kutoa kipaumbele
kwa wazee wote nchini wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma.
Waziri
Ummy akiwasalimia wazazi waliolazwa kwenye moja ya wodi Hospitali ya
Meta kutokana na ufinyu wa wodi inawalazimu akinamama wengine kulala
chini hospitali hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa jengo jipya ambalo
litaondoa msongamano wa wazazi hospitalini hapo.
Waziri wa Afya akiwasalimia wagonjwa waliofika Hospitali ya Uzazi ya Meta kupata matibabu.
TRA Yakamata Bidhaa Za Magendo, Ni Sukari Na Mafuta Ya Kula
Nyumba
hii ndiyo Ofisi ya Bosi ambayo utumika kuweka bidhaa kabla ya
kusambazwa sokoni iliyopo Somanga njia nne eneo la Kikanda Wilaya ya
Kilwa mkoa wa Lindi.
sehemu ya kuweka sukari na kupima.
Nyumba inayotumika kuweka sukari
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayomboakionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.
Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.
Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba
Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akionesha sukari.
Aina ya mafuta kutoka nje ya nchi tayari kuwekwa kwenye ndoo kwa kupeleka Sokoni
Polisi akilinda viroba vyenye sukari kutoka nje ya nchi.
Madumu yaliyokua na mafuta ya kula na ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta
Nyumba ya mtuhumiwa Yusuf Sareh iliyopo Somanga Njia nne Kikanda.
………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu-Kilwa
Siku
ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha
(FAST) wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la
kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara Yusuf Barkat Sareh, Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu. Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo.
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko762 Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135
Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49 Betri aina ya tigger katoni 223 Amira katoni 135
Sabuni za kufulia katoni 48 Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari.
Mashine
mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya
nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini nya sukari vya
Kilombero,TPC na Mtibwa Sugar. Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India 2000 Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari36,000 mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo25 kiasi cha 1150 Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609 Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.
Waziri Ummy mwalimu atembela hospitali mbeya
Hospitali zinazotumia mfumo.wa ukusanyaji mapato wa kielectronik wametakiwa wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.
Rai
hiyo.imetolewa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda
ya mjini Mbeya
Ummy
alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa
katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo Ununuzi wa dawa,vifaa na
vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa Watumishi
“Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote,tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa”alisema
Aidha alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa
itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma,hivyo
wameishauri bohari kuu ya dawa wanunue dawa toka kwa wawekezaji Wa hapa
nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji wa
dawa kwa haraka
waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia,kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa
“Tunao watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa Na
kuzipeleka kwenye maduka ya.dawa binafsi,hao hatutowafumbia macho na
kuwapeleka mahakamani”
Kuhusu upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini ,Wazirini wa Afya
alisema,nchi ina upungufu wa asilimia 52,hivyo.serikali inatarajia
kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa
nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni
Katika hospitali ya uzazi ya Meta,waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi
za wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na
wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka
ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na
watoto njiti
Hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha
shilingi mia tano,inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya
watu milioni mbili.
No comments:
Post a Comment