Sunday, 10 April 2016

Wananchi wa Ushirika Tukuyu Wazuiliwa kujenga Zahanati

1Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi hao ambao waliomzunguka kutoa kero yao ya kuzuiwa kuendelea na ujenzi wa zahanati.
4Wananchi wa kata ya Ushirika-Tukuyu wakiwa wamebeba bango kuonesha kilio chao kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto.
2 3Mmoja wa mwanakamati akimueleza mgogoro wao wa eneo la ujenzi wa zahanati kati yao na mkurugenzi wa halmashauri yao.

Na.Tabu Mullah

Wananchi wa kata ya ushirika wilayani tukuyu wameusimamisha msafara wa waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto uliokua ukitoka wilayani kyela kuelekea mbarali kwa madai hawana kituo cha afya wala zahanati kwa miaka hamsini sasa.

Wananchi hao ambao walikua wameshika bango kubwa lililoandika hawamtaki mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa madai ya kuwasimamisha ujenzi mara mbili
Akieleza kilio chao katibu.wa kamati ya ujenzi  bi.fatma mwandegele alisema eneo hilo limeingia kwenye mgogoro wa ardhi kwa muda mrefu kati ya kijiji cha mpunguso na aliyekua katibu tarafa wa kata ya pakati bw.mwakapala

Hatahivyo alisema kesi kuhusu eneo hilo ilishamalizika na wananchi walikusanya nguvu zao kwa kuchangia simenti na mawe hata hivyo simenti hiyo iliharibika

Waziri Ummy Mwalimu ilimrazimu kwenda kuliona eneo hilo ambalo  limechimbwa tayari kwa kuanza msingi huku mawe yakiwa yamerundikwa pasipo kuendelea na ujenzi alimuagiza mganga Mkuu wa mkoa ambaye alikua nae kwenye msafara wake,siku ya jumatatu wafike eneo hilo Pamoja na mkurugenzi na mganga mkuu wa wilaya ili waeleze kwanini wasiendelee na ujenzi wa zahanati hiyo.

“Nawaomba wananchi muwe watulivu ili tujihakikishie kama kesi hiyo imekwisha na kwanini Tusiendelee na ujenzi huu na jumatatu kabla ya.saa tisa mchana niwe nimepata ripoti ya eneo hili
Aidha,Waziri huyo aliwathibitishia wananchi hao kwamba lazima zahanati ijengwe kwenye kijiji Hicho ili kiweze kuwahudumia wananchi na kuwaahidi.serikali itawaletea wahudumu pamoja na dawa,vifaa na vifaa tiba.

Waziri Ummy  Mwalimu Ameahidi  Kuwapelekea  Dawa Za  Kutibu Maji (Water Guard) Wananchi  Wa Kyela.

1Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto akisalimiana na watoa huduma wa hospitali ya wilaya ya kyela.
2Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya wilaya wakimsubiri kumpokea waziri wa afya.Mh.Ummy Mwalimu amewakumbusha watoa huduma hao kuwahudumia wananchi kwa kufuata weledi wa taaluma zao.
5Waziri Ummy Mwalimu akipata maelezo kwenye dirisha la wanaotumia kadi ya mfuko wa wa jamii(CHF) Toka kwa mhudumu(hayupo pichani)wa hospitali ya wilaya ya kyela.
3Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na watendaji wa wilaya ya Kyela,kushoto ni makamu mwenyekiti wa Wilaya Stephen Mwangalaba,na kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo dkt. Thea Ntara.
4Mkuu wa Wilaya ya Kyela dkt.Thea Ntara akitoa taarifa ya wilaya kwa waziri wa afya,maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,alipotembelea hospitali ya wilaya ya kyela.

No comments:

Post a Comment