Pigano la Marudio
kati ya Tyson Fury na Wladmir Klitschko litaandaliwa Mjini Manchester Mnamo mwezi Julai Tarehe 9 kulingana na Mkufunzi wa Bondia Huyo wa
Uingereza.
Mabondia hao Wawili Wakikabiliana katika Pigano la kwanza
Fury ambaye ni Mzaliwa wa Mjini Manchester na ambaye ana Umri wa Miaka 27,alimshinda Raia wa Ukraine Klitschko kwa pointi mjini Dusseldorf mwezi Novemba ili kushinda mikanda Mitatu ya WBA,IBF na WBO.
Ushindi huo Unamaanisha kwamba Fury ni Muingereza wa Tano kushinda Mataji Hayo ya Uzani Mzito zaidi Duniani.
Taji hilo litakuwa Wazi Siku ya Jumamosi ambapo mshindi wa medali ya Dhahabu katika Shindano la Olimpiki Anthony Joshua atakabiliana na Bingwa Mtetezi Charles Martin katika Ukumbi wa 02 mjini London.
No comments:
Post a Comment