Michezo Minne ya Robo fainali ya Michuano ya Europa ligi imechezwa katika Viwanja Vinne Tofauti.
Sevilla Wakawachapa ndugu Zao wa Athletic Bilbao kwa Mabao 2-1mabao ya Ushindi ya Sevilla Yakifungwa na Timothee Kolodziejczak na Vicente Iborra, Huku bao la kufutia Machozi la Bilbao likifungwa na Aduriz Zubeldia.
Sporting Braga wakiwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk walikubali kulala kwa kichapo cha Mabao 2-1,Wachezaji Yaloslav Rakitskiy na Facundo Ferreyra Wakifunga Mabao ya Ushindi, Huku Naval Costa Eduardo kwa Braga.
Villarreal Wakicheza katika Dimba la El Madrigal Walichomoza na Ushindi wa Mabao 2-1 Dhidi Ya Sparta Prague, Cedric Bakambu akifunga Mabao Yote Mawili kwa Upande Villareal Huku Jakub Brabec Akifunga Bao Pekee la Sparta.
No comments:
Post a Comment