Monday, 11 April 2016

Droo ya Nusu Fainali kombe la Shirikisho Kesho

Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), inatarajiwa kufanyika kesho Jumanne saa 3 usiku moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo.
Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itafanyika live katika kituo cha AzamTwo, ambao kupitia Azamtv ndio wadhamini wa wakuu wa michuano hiyo iliyoibua Msisimiko wa mpira wa miguu na kushirikisha timu nyingi zaidi nchini.

Baada ya timu za Azam FC, Mwadui FC, na Yanga SC kukata tiketi ya kucheza Nusu Fainali, Mshindi wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Coastal Union utakaochezwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam atungana na timu hizo tatu kwenye droo ya kesho.

Michuano ya Kombe la Shirikisho iliyoanza kwa kushirikisha timu 64 mwishoni mwa mwaka Jana, imefikia hatua hatua ya nusu fainali, baada ya Azam FC kuindoa Prisons (3-1), Mwadui FC kuiondosha Geita Gold (3-0) na Yanga SC kuwaondoa Ndanda FC kwa mabao (2-1).

Mshindi wa Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu huu, ataiwakilisha Tanzania mwaka 2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).

Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuimarisha Miundombinu na mazingira rafiki kwa Wafanyakazi Wake

11 (1)
Na Mwandishi wetu , Zanzibar.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuimarisha Miundombinu na Mazingira rafiki ya kiutendaji kwa kuwapatia vifaa vya kisasa jumuiya mbali mbali za taasisi hiyo ili zifanye kazi kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar, Najma Murtaza Giga wakati akikabidhi Vifaa mbali mbali kwa Uongozi wa Wazazi Mkoa wa Mjini, huko Afisi ya CCM Amani.

Amesema taasisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na mabadilio ya sayansi na teknolojia kwa kutumia nyenzo za 

kisasa zitakazowasaidia watendaji wa taasisi hizo kufanya kazi nzuri na kwa haraka.
Aidha amesema chama hicho kitafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kinawapatia Vitendea Kazi Watendaji wa CCM kadri ya uwezo wa kifedha unaporuhusu.

Giga amewasihi viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zingine kuunga mkono juhudi Zinazofanywa na jumuiya ya wazazi katika kutoa malezi bora ya kitaaluma na kisaikolojia kwa watoto kwa lengo la kutengeneza viongozi makini na weledi wa baadae.

Nae Katibu wa CCM mkoa wa mjini, Mohamed Omar Nyawenga amewataka watendaji wa Chama hicho kuwa wabunifu na kutumia weledi kwa kufanya kazi kwa bidi ili kusaiudia Chama kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 kwa ufanisi ili wananchi waendelee kuiunga mkono CCM katika chaguzi zote zijazo.

Vifaa vilivyotolewa ni Komputa 2, mashine za Printer 2 na mashine za photocopy 4 kwa Jumuiya ya wazazi mkoa wa mjini kichama.

No comments:

Post a Comment