Wednesday, 16 November 2016

Trump ataka alipwe dola moja tu kila mwaka

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000 atakapochukua hatamu Januari mwakani. Badala yake atakuwa akilipwa dola moja ya Marekani ($1) pekee kila mwaka  sawa na shilingi 2000 ya kitanzania.
Tokeo la picha la 1 us dollar
Alifichua mpango wake huo wakati wa mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes cha CBS News.
Ingawa hakujua rais huwa analipwa pesa ngapi, Bw Trump alisema alidhani anahitaji kuchukua tu $1.
Baada ya Bi Stahl kumjulisha kwamba mshahara wa rais ni $400,000, alisema: "Hapana, sitaupokea mshahara huo. Sizichukui kamwe."
Rais huyo mteule anatimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni.Tokeo la picha la 1 us dollar vs donald trump
Aliambia waliohudhura mkutano wake Septemba kwamba mshahara wa rais si jambo kubwa kwake.

Kuna viongozi wengine walioukataa mshahara?

Bw Trump si kiongozi wa kwanza wa Marekani kukataa mshahara.
Herbert Hoover, aliyekuwa ametajirika kupitia biashara ya madini kabla ya kuingia madarakani, na John F Kennedy, aliyerithi utajiri mwili, wote walikataa kupokea mashahara na badala yake wakatoa pesa hizo zisaidie wasiojiweza katika jamii.
Meya wa zamani Michael Bloomberg, gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger na gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney pia walikataa kupokea mishahara yao.
Mark Zuckerberg, mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, ndiye mfanyakazi anayelipwa mshahara wa chini zaidi katika kampuni hiyo.
Aidha, ni miongoni wa CEO (Afisa Mkuu Mtendaji) wengi ambao hulipwa mshahara wa $1 pekee.

No comments:

Post a Comment