Muhubiri maarufu wa vipindi vya Televisheni nchini Nigeria TB Joshua
amesema ametabiri " kwamba Hillary Clinton atamshinda Donald Trump"
katika uchaguzi wa urais wenye ushindani mkali tarehe 8 Novemba mwaka
huu.
Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook TB Joshua
amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo, lakini atakabiliwa
na changamoto nyingini - likiwemo jaribio la kupiga kwa kura ya kutokuwa
na imani dhidi yake.
"boti ya rais mpya itakuwa imefungwa," aliongeza.
TB Joshua ni mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi na utata barani
Afrika, huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa "utabiri " wake ni wa
uhakika.
No comments:
Post a Comment