Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoamuhtasari wa matokeo ya
Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015,
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Damian Lubuva (kushoto) akitoamaenelezo ya
Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015,
mjini Dodoma.
Mwenyekitiwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhiWaziri wa
Nchi Ofisi ya WaziriMkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
WalemavuMhe. JenistaMuhagama (kulia) Taarifa ya TathminiBaada ya
Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwaniwamwaka 2015, mjini Dodoma.
Mwenyekitiwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Damian Lubuva (kushoto) na Waziri wa Nchi
Ofisi ya WaziriMkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na WalemavuMhe.
JenistaMuhagama, wakioneshaVitabu vya Taarifa ya TathminiBaada ya
Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwanimwaka 2015, mjini Dodoma.
Waziriwa Nchi Ofisi ya
WaziriMkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na WalemavuMhe.
JenistaMuhagamaakihutubiamkutano wa kukabidhi Taarifa ya Tathmini ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwaniwamwaka 2015, mjini
Dodoma.Kushoto niMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
JajiMstaafu Damian Lubuvana kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mst.
wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid.
Pichana Hussein Makame, NEC
Wahenga walisema “Safari bila ya
dira huishia kupotea njia”. Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015, Tume ya Taifa ya uchaguzi iliamua Kufanya tathmini ili
kubaini utekelezaji wa uchaguzi mkuu.Katika utekelezaji wa mkakati
wowote ni muhimu kuwa na dira ili kujua mafanikio au kushindwa kwa
utekelezaji wa mkakati huo.
Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi
Mkuu wa Mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilifanya tathmini ya
Uchaguzi huo katika halmashauri 75 kwa kuwahoji na kujadiliana na wadau
mbalimbali wa uchaguzi ili kupata mtazamo wao juu ya Uchaguzi huo.
Oktoba 28 mwaka huu, NEC
imekabidhi Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani wa Mwaka 2015 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama kwa
niaba ya Serikali, kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva anasema Tathmini
hiyo imefanyika kuanzia tarehe 1 hadi 26 mwezi Februari, 2016 katika
Mikoa 22 kati ya mikoa 30 iliyokuwepo wakati wa Uchaguzi huo,
Halmashauri 64 kati ya 181, Kata 192 kati ya 3,953 za Tanzania Bara na
Shehia 12 kati ya 386 za Tanzania Zanzibar.
Anabainisha kuwa lengo kuu la
tathmini hiyo ni kupata mtazamo wa wadau juu ya taswira halisi ya Tume
ili kujenga msingi bora wa kutekeleza chaguzi zijazo na kupata majibu ya
changamoto zilizojitokeza kwenye Uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kujua
kwa nini baadhi ya maeneo yalikuwa na mwitikio mdogo wa kupiga kura
ikilinganishwa na wapiga kura waliojiandikisha.
“Matokeo ya tathmini hii pia
yataisaidia Tume katika kujitathmini katika maeneo ya kiutendaji ikiwamo
kurekebisha Sheria, Kanuni, masuala ya kisera na kufanya mapitio ya
Mpango Mkakati wa Tume na Mkataba wa Huduma kwa Mteja” anasema Jaji Mst.
Lubuva.
Akizungumzia Tahmini hiyo,
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima
Ramadhani anasema takwimu za tathmini hiyo zimekusanywa kupitia
mahojiano ya ana kwa ana kwa msaada wa madodoso na majadiliano ya makundi maalumu.
Anasema majadiliano yalijumuisha
makundi maalum 192 ya wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 na makundi 192
ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 na kila kundi lilijumuisha
kati ya watu 5 hadi 10 kwa kuzingatia jinsi pamoja na watu wenye
ulemavu.
Bw. Kailima anabainisha kuwa
sampuli ya watu waliohojiwa ilikuwa watu 1,915 ambapo kati yao 1,029
walikuwa Watendaji wa Uchaguzi, 499 wapiga kura na watumishi wa umma
walikuwa 387 na kati yao wanaume walikuwa 1,184 sawa na asilimia 62 huku
wanawake wakiwa 731 sawa na asilimia 38.
Kwa upande wa umri, Bw. Kailima
anasema sampuli hiyo ilikuwa na vijana (miaka 18 – 35) 767 sawa na
asilimia 40, umri kati ya miaka 36 – 60 walikuwa 1,085 sawa na asilimia
57 na umri zaidi ya miaka 60 walikuwa 63 sawa na asilimia 6.
Kwa mujibu wa Jaji Mst. Lubuva,
wadau waliohojiwa ni pamoja na Watendaji wa Uchaguzi katika Ngazi
mbalimbali wakiwemo Wasimamizi wa Uchaguzi, Makarani wa Uchaguzi,
Makarani waongozaji, wasimamizi wa Vituo, Wasimamizi wasaidizi na
Walinzi wa Vituo, Wapiga Kura, wananchi wa kawaida.
Bw. Kailima anasema kati ya wadau
1,915 waliohojiwa, wadau 727 sawa na asilimia 38 walitoka katika maeneo
yaliyokuwa na mwitikio mkubwa, wahojiwa 238 sawa na asilimia 12
walitoka katika maeneo yaliyokuwa na mwitikio wa wastani na 950 sawa na
asilimia 50 walitoka katika maeneo yaliyokuwa na mwitikio Mdog
Akitoa muhtasari wa matokeo ya tathmini hiyo kwa baadhi ya maeneo, Bw. Kailima anasemakuhusu
Utaratibu wa Kupiga na Kuhesabu Kura, matokeo yanaonesha kuwa, jumla ya
Watendaji na Wadau wa Uchaguzi 1,915 waliohojiwa, 1,895 sawa na
asilimia 99 walibainisha kuwa taratibu zilifuatwa.
Kuhusu Kujumlisha Kura,jumla ya
Watendaji wa Uchaguzi 1,029 walihojiwa, kati yao Watendaji 1,023 sawa na
asilimia 99.4 walieleza kuwa, taratibu za Uchaguzi katika kujumlisha
Matokeo zilifuatwa..” anasema Bw. Kailima
Kuhusu Taratibu za Kutangaza
Matokeo, Bw. Kailima anasema matokeo yanaonesha kuwa, kati ya Watendaji
1,029 waliohojiwa, 1,003 sawa na asilimia 97.5 walisema taratibu
zilizingatiwa katika kutangaza matokeo.
Kutokana na matokeo ya Tathmini
hiyo, Jaji Mst. Lubuva anasema Tume imejiridhisha kupitia maoni ya wadau
kwamba Sheria, Kanuni na maelekezo yaliyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu
yalikuwa chachu ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu.
“Aidha, wadau wengi walionesha
kuridhishwa na utendaji wa Tume katika kusimamia Uchaguzi Mkuu na
kutangaza matokeo kwa kufuata Sheria na Kanuni zilizopo” anasema Jaji
Mst. Lubuva.
Kuhusu mwitiko wa Wapiga Kura,
Jaji Mst. Lubuva anasema kuwa Tathmini imeonesha kuwa katika baadhi ya
maeneo watu waliojitokeza kupiga Kura ni wachache ikilinganishwa na
idadi ya Wapiga Kura waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura.
Akitaja sababu za hali hiyo, Jaji
Mst. Lubuva anasema ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kupiga
kura kutokana na Elimu ya Mpiga Kura kutowafikia wapiga Kura wengi,
Wapiga Kura walijiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili
kupata Kadi kwa ajili ya matumizi mengine na kuwepo hofu ya vitisho na
vurugu siku ya kupiga Kura.
Ili kukabiliana na changamoto
mbalimbali zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo, Jaji Mst. Lubuva anasema
wadau wamependekeza mambo mbalimbali ikiwemo Uboreshaji endelevu wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuitaka Serikali itenge fedha za
kutosha kwa ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura kila mwaka.
“Wadau wamependekeza kuwa
Serikali ifanye mapitio ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 na
Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura 292 ili kurekebisha vifungu
vinavyokinzana; na Serikali ibadili Muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
ili kuwa na Ofisi na Watumishi katika kila Halmashauri nchini na Ofisi
Zanzibar” anasema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama
anasema baada ya kupata maelezo ya matokeo ya tathmini, anashawishika
kusema kuwa kwa kiasi kikubwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitekeleza
majukumu yake ya Kikatiba kwa ufanisi mkubwa.
“Huu ni mfano na funzo kuwa
Watanzania tukiamua kutimiza wajibu wetu kwa maslahi mapana ya Nchi
hatutashindwa. Kinachotakiwa ni kuwa na dhamira ya dhati ya kufanikiwa
kwa kila jambo tunalopanga kulitekeleza” anasema Waziri Mhagama.
Anaongeza kuwa kifungu cha 15 (5)
cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura 343, Tume kinaagiza kuboresha
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja
na mwingine, hata hivyo haikuwezekana kufanyika hivyo baina ya mwaka
2010 na mwaka 2015 kutokana na ufinyu wa Bajeti na kuchelewa kupatikana
fedha kwa wakati.
“Kutokana na hali hiyo, naomba
niseme kuwa Serikali itahakikisha kuwa, upungufu uliojitokeza
unatatuliwa kwa kadri ya uwezo wetu ili kuiwezeshwa Tume kutekeleza
majukumu yake ya Kikatiba na Kisheria kwa ufanisi na kwa wakati”
Akizungumzia Elimu ya Mpiga Kura,
Bw. Kailima anasema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina wajibu wa Kisheria na
Kikanuni wa kutoa Elimu ya Mpiga Kura, Kuratibu na Kusimamia watu na
Taasisi zinazotaka kutoa Elimu hiyo.
Anasema uzoefu unaonesha elimu ya
Mpiga Kura hutolewa wakati wa Uchaguzi Mkuu na hasa kipindi baada ya
Uteuzi wa Wagombea na hukoma mwisho wa Kampeni za Uchaguzi huku Taasisi
na Asasi zinazotoa elimu hiyo nazo zikiomba kibali cha kutoa elimu hiyo
kipindi cha uchaguzi tu.
Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi
anasema ili kutekeleza matakwa ya Sheria, Tume itatoa Elimu ya Mpiga
Kura kwenye maonesho mbalimbali, Mikutano inayojumuisha wadau wa
Uchaguzi na kwenye Shule za Sekondari na vyuo vikuu nchini.
Anasema hadi sasa Tume imeshatoa
Elimu hiyo kwenye maonesho ya Sabasaba, Nanenane, Mkutano Mkuu wa
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania, Wiki ya Vijana Kitaifa, na
kutembelea Shule za Sekondari za Wilaya za Kondoa (Dodoma), Uvinza
(Kigoma), Ubungo (Dar es salaam), Manispaa ya Musoma (Mara), na Mji wa
Bariadi mkoani Simiyu.
Mbali na njia hizo, anaongeza
kuwa Tume itatoa Elimu hiyo kwa kuhudhuria na kutoka Elimu hiyo katika
Mikutano ya Viongozi wa Dini, Kamati za Ushauri za Mikoa na Wilaya,
Mabaraza ya Madiwani na Mikutano Mikuu ya Vijiji na Mitaa.
“Aidha Tume itahudhuria na kutoa
Elimu ya Mpiga Kura katika vikao au mikutano itakayowajumuisha viongozi
mbalimbali kama Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Wakuu,
Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya na Jeshi la Polisi” anasema Bw.
Kailima na kuongeza kuwa:
“Tume pia itaanzisha klabu za
Uchaguzi katika shule za Sekondari angalau moja kwa kila Mkoa kwa
kuanzia. Lengo likiwa ifikapo mwaka 2019, kila Wilaya katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania iwe na Klabu ya uchaguzi katika shule moja ya
Sekondari”
“Tume itatembelea vyombo vya
habari na kukutana na watumishi wake, na vipindi mbalimbali vya Luninga
na Radio na kuzichapisha makala katika magazeti na mitandao ya Kijamii
na kutoa vibali vya kutoa elimu ya Mpiga Kura kwa Taasisi na Asasi”
Bw. Kailima anaamini kuwa Elimu
ya Mpiga Kura ikitolewa katika kipindi chote cha mwaka itawezesha
wananchi na wadau kupata taarifa sahihi kuhusu Tume, Kazi, Wajibu na
Majukumu yake, kufahamu utaratibu wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.
Anasema kupitia Elimu hiyo,
wananchi na wadau watafahamu taratibu na hatua zote za Uchaguzi hadi
kutangaza matokeo na kujua umuhimu na thamani ya wao kushiriki katika
shughuli za mchakato mzima wa Uchaguzi na kuzingatia taratibu zote.
No comments:
Post a Comment