Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta
anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumatano kujiunga na kikosi cha timu
hiyo kwa ajili yaa mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe mwishoni mwa
wiki.
Samatta amesema kwamba
anaondoka leo Genk, Ubelgiji kupitia Dubai ambako atalala siku mbili
kabla ya kuunganisha safari ya kuja Dar es Salaam.
Samatta ameendelea kuonyesha umuhimu wa kuichezea Taifa Stars kwa
kuitikia wito wa kocha Charles Boniface Mkwasa licha ya kuwa na majukumu
mazito katika klabu yake.
Mbwana Samatta (kushoto) anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumatano kujiunga na Taifa Stars
Wachezaji 24 walioitwa na Mkwasa kwa ajili ya mchezo huo wa Novemba 13 mjini Harare, wataingia kambini Novemba 7, mwaka huu.
Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’
wa Yanga, Said Kipao wa JKT Ruvu na Aishi Manula wa Azam FC.
Mabeki; Erasto Nyoni, David Mwantika wa Azam FC, Michael Aidan wa JKT
Ruvu, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew wa Yanga, Mohammed Hussein
‘Tshabalala’ wa Simba SC na James Josephat wa Prisons.
Viungo wa kati ni Himid Mao wa Azam FC, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Jonas
Mkude na Muzamil Yassin wa Simba SC, wakati viungo wa pembeni ni
Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, Shizza Kichuya, Jamal Mnyate wa
Simba SC na Simon Msuva wa Yanga.
Washambuliaji ni Ibrahim Hajib wa Simba SC, John Bocco wa Azam FC, Elius
Maguli wa Oman Club, Thomas Ulimwengu aliyemaliza mkataba wake TP
Mazembe ya DRC na kundoka mwezi uliopita, Omar Mponda wa Ndanda FC na
Nahodha Mbwana Samatta wa K.R.C Genk ya Ubelgiji.
No comments:
Post a Comment