Mkuu wa wilaya ya ilala mhe. Sophia mjema atekeleza agizo la rais kwa vitendo
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akitembelea barabara ya
Lumumba jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya eneo ambalo wamelitenga
kwa ajili ya Wamachinga kufanya biashara zao siku za Ijumaa, Jumamosi na
Jumapili. Amewapongeza baadhi ya Wamachinga waliojitokeza eneo hilo na
kuwataka wengine kujiandikisha na kuchangamkia fursa hiyo yenye tija
kwao. Mhe Dc aliongozana na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Msongela Palela,
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni. na Katibu
Tawala wa Wilala ya Ilala Edward Mpogolo
Baadhi ya wafanyabiashara wakijiandishi majini yao ili wapatiwe
maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki,
leo jijini Dar es Salam.
Baadhi ya wafanyabiashara waliojitokeza katika eneo hilo wakiendelea na kazi
Baadhi ya wananchi wakiwa katika barabara ya Lumumba wakijipatia
mahitaji yao ikiwa ni moja ya eneo ambalo wamelitenga kwa ajili ya
machinga kufanya biashara zao.
Wafanyabiashara waliojitokeza wakiweka alama katika eneo hilo
Kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli kuwataka viongozi kuwatafutia
maeno ya kufanyia biashara Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama
Machinga na ikiwezekana wapewe fursa ya kuzitumia baadhi ya barabara kwa
shughuli hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema ameanza
kutekeleza agizo hilo kwa vitendo.
Akiwa mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Mkuu wa Wilaya huyo
amewapongeza baadhi ya machinga waliojitokeza eneo hilo lililotengwa
kwa ajili yao na kuwataka wengine kujiandikisha na kuchangamkia fursa
hiyo yenye tija kwao.
No comments:
Post a Comment