Na.Alex Mathias.
Licha ya kuwa ugenini timu ya
Taifa ya Brazil imeisambaratisha Peru jumla ya magoli 2-0 mchezo wa
kufuzu kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi uliochezwa katika uwanja
wa Estadio Nacional uliopo mji wa Lima nchini Peru.
Timu ya Peru walionekana kuwabana
vilivyo Brazil kwa style yao ya kushambulia na kujilinda na kufanya
timu hizo ziende mapumziko zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa
Brazil kujaruka na kushambulia kwa kasi na kwa lengo la kupata pointi
tatu muhimu ambazo zitawarahishia kwenda Urusi mapema alikuwa
mshambuliaji Jesus Gabriel dakika ya 58 alifunga goli la kwanza na
Renato Augusto aliipatia goli la pili Brazil na kuonesha njia nyeupe ya
kufuzu michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo Brazil
wamendelea kung’ang’ania kileleni mwa msimamao wakiwa na pointi 27 na
kujiweka katika hatua nzuri ya kuwapeleka nchini Urusi mwaka 2018 wakati
Peru wanaonekana kupoteza matumaini ya kufuzu kwani wapo katika nafasi
ya nane wakiwa na pointi 14.
Brazil watakuwa ugenini Machi
24,2017 kucheza na Timu ya Uruguay ya Luis Suarez ambayo imepoteza
mchezo wake dhidi ya Argentina ya Lionel Messi.
No comments:
Post a Comment